Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atasema:
“Ee Mola Wangu, Maswahabah zangu!” Halafu aambiwe:
“Walibaki ni wenye kuritadi tangu ulipofarakana nao.”
Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aseme:
“Watokomee! Watokomee!”
Raafidhwah wenye kusema kuwa Maswahabah wote wameritadi kutoka katika Uislamu wameshikamana na andiko hili. Miongoni mwao ni Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum). Kuhusiana na ´Aliy na watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wao wanasema kuwa hawakuritadi kwa madai yao.
Ni jambo lisilokuwa na shaka kwa madai haya wamesema uongo. Makhaliyfah wote wanne hakuna yeyote katika wao aliyepitikiwa na kuritadi kwa makubaliano ya waislamu wote. Vilevile Maswahabah wote wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakupitikiwa na kuritadi kwa makubaliano ya waislamu wote. Isipokuwa tu watu katika mabedui ambao walikuwa ni wepya katika Uislamu. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokufa wakarudi nyuma na kuritadi na kukataa kutoa zakaah mpaka Khaliyfah mwongofu Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) akawapiga vita na wengi wao wakawa wamerudi katika Uislamu. Hata hivyo Raafidhwah kutokana na ukubwa wa vifundo vyao na chuki yao kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakashikamana na uinje wa Hadiyth hii.
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuhusiana na Hadiyth hii wanasema kuwa imeenea na inachokusudia ni umaalum. Kuna maandiko mengi ambayo yameenea na kunakusudiwa umaalum. Neno lake:
“Maswahabah zangu”
Hakukusudiwi kuwa ni wote. Hawa inahusu wale walioritadi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliambiwa:

Ni jambo lenye kujulikana kuwa Makhaliyfah waongofu na Maswahabah wote wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakuritadi kwa makubaliano ya waislamu. Lau tungelikadiria kuwa waliritadi tusingelibaki na uaminifu wowote juu ya Shari´ah. Kutokana na hili kuwatukana Maswahabah kunalazimisha pia kuitukana Shari´ah ya Allaah, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Allaah, Mola wa walimwengu. Wale wenye kuwatukana Maswahabah kunalazimisha katika kufanya hivo madhara manne na maovu makubwa:
– Kuwatukana Maswahabah.
– Kuitukana Shari´ah.
– Kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
– Kumtukana Mola wa walimwengu.
Lakini pamoja na hivyo ni vijitu visivyoelewa:
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
”Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[1]
1 – Ni kuitukana Shari´ah kwa sababu ambao wametupokelea Shari´ah ni Maswahabah. Ikiwa waliritadi na Shari´ah imekuja kupitia wao ina maana haikubaliwi. Kafiri khabari zake hazikubaliwi. Bali hata Faasiq. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا
“Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni.”[2]
2 – Ni kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ikishakuwa hali ya Maswahabah wa Mtume wana ukafiri na ususaki iko namna hii basi ni lazima vilevile yamguse Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu mtu huwa katika dini ya rafiki yake. Mtu yeyote hutiwa kasoro kwa kumwangalia rafiki yake ikiwa kama rafiki yake ni mbaya. Husemwa ya kwamba fulani sio mtu mzuri kwa kuwa marafiki zake ni fulani na fulani. Hivyo kuwatukana Maswahabah ni kumtukana yule aliyesuhubiana nao.
3 – Kusema kuwa ni kumtukana Allaah, Mola wa walimwengu, ni jambo liko wazi sana. Ni kwa kule Yeye kufanya ujumbe huu ambao ndio bora zaidi na unaowahusu viumbe wote kupitia mikono ya Maswahabah hawa. Ukiongezea juu ya hilo Yeye afanye Maswahabah wa Mtume huyu ambaye ndiye Mtume bora (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ambavo wanavodai Raafidhwah hawa ya kwamba waliritadi.
Tunaamini kuwa huu ni uongo mkubwa juu ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na ni kumfanyia uadui Allaah, Mtume Wake na Shari´ah ya Allaah.
Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba sisi tunawapenda Maswahabah wote wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na watu wa kwa nyumba ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wale ambao ni waumini. Tunaonelea kuwa watu wa kwa nyumba yake wana haki mbili:
1 – Haki ya kule kuamini.
2 – Haki ya udugu wao na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 02:171
[2] 49:06
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/309-311)
- Imechapishwa: 05/01/2025

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/309-311)
Imechapishwa: 05/01/2025
https://firqatunnajia.com/matusi-dhidi-ya-shariah-mtume-na-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)