Madhara ya saba ni kuwa Bid´ah inafarikanisha Ummah wa Kiislamu. Ummah wa Kiislamu ukifunguliwa mlango wa kuzusha Bid´ah, itakuwa kila mmoja anazusha alitakalo kama ifanywavyo leo. Ummah wa Kiislamu inakuwa kila kipote kinafurahia yale waliyomo:
كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
“Kila kundi kwa yaliyonayo linafurahia.” (30:32)
Kila kipote kitasema wao ndio wanafuata haki na wengine ni wapotevu. Allaah amemwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
“Hakika wale walioefarikisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna lolote kuhusiana na wao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya. Atakayekuja [Siku ya Qiyaamah] kwa [jema] basi atapata [thawabu] kumi mithali wa hilo. Na Atakayekuja kwa uovu, basi hatolipwa ila mithali wa hilo, nao hawatodhulumiwa.” (06:159-160)
Watu wakishaanza kuzusha Bid´ah watatofautiana na itakuwa kila mmoja anasema kuwa yeye ndiye mwenye kufuata haki na fulani ni mpotevu na kumtuhumu uongo, uzushi, makusudio mabaya na kadhalika.
Tupige mfano wale waliozusha usherehekeaji wa kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakawa wanasherehekea siku ambayo wanadai kuwa amezaliwa ambayo ni tarehe 12 Rabiy´ al-Awwaal. Hivi mnajua wanayosema juu ya wale wasiofanya Bid´ah hii? Wanasema kuwa watu hawa wanambughudhi na kumchukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio sababu inawafanya kutofurahikia kuzaliwa kwake, hawasherehekei na mfano wa hayo. Utawaona ni wenye kuwatuhumu watu wa haki kwa jambo ambalo wao ndio wenye haki zaidi ya kulisema kuliko wao.
Uhakika wa mambo ni kwamba mtu mwenye kuzusha Bid´ah hilo linapelekea kumchukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama atadai kuwa anampenda. Kwa sababu akizusha Bid´ah hii ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwawekea nayo Ummah, ni kama nilivowaambia huko mbeleni, ima anamtuhumu kuwa hakuijua au alifanya khiyana.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/330-331)
- Imechapishwa: 05/01/2025

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/330-331)
Imechapishwa: 05/01/2025
https://firqatunnajia.com/mnajua-ahl-ul-bidah-wanavowatuhumu-salafiyyuun-kwa-kutosherehekea-maulidi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)