Matibabu ya meno yanafaa, lakini sio kutia mwanya

Swali: Kuna mwanamke ambaye anayo kasoro ya kimaumbile katika meno yake. Je, inafaa kwake kujitibisha na kuweka sawa?

Jibu: Ndio, hapana vibaya ikiwa ni matibabu. Kilichokatazwa ni kutia mwanya.

Swali: Je, inafaa kung´oa jino lililozidi katika ufizi?

Jibu: Ndio, ikiwa manufaa yamepelekea kufanya hivo. Huku sio kutia mwanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23545/هل-يجوز-علاج-الاسنان-بالتقويم-والتسوية
  • Imechapishwa: 09/02/2024