Fatwa ya kundi la Maswahabah pindi mwenye hedhi anaposafika baada ya ´Ishaa na baada ya ´Aswr

Swali: Je, analazimika mwanamke kuswali Maghrib na ´Ishaa akitwahirika dakika 30 kabla ya kupambazuka Fajr?

Jibu: Haya yameyatolea fatwa jopo la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ni kama ambavo akisafika wakati wa alasiri ataswali Dhuhr na ´Aswr. Huu ni wakati wa dharurah. Baada ya nusu ya usiku ni wakati wa dharurah. Ni mfano wake vivyo hivyo kuhusu wakati wa alasiri.

Swali: Ni ipi fatwa yako juu ya suala hilo?

Jibu: Ataswali Maghrib na ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23547/حكم-المغرب-والعشاء-لمن-طهرت-قبل-الفجر
  • Imechapishwa: 09/02/2024