Swali: Je, mwanamke azingatie damu anayoiona baada ya kumaliza hedhi yake?

Jibu: Hapana, inakuwa ni damu ya kawaida inayokuja baada ya ada yake. Atatawadha kwa ajili ya kila swalah.

Swali: Hata kama ni damu ya hedhi?

Jibu: Ikiwa ni baada ya ada yake ni damu inayowapata wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehukumu kwa kuzingatia ada ili wanawake wapate kupumzika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23548/هل-تعتد-المراة-بالدم-الذي-تراه-بعد-الحيضة
  • Imechapishwa: 09/02/2024