Matendo ya waislamu ndio yanawafanya makafiri kutoingia Uislamu

Kusafiri kwenda katika miji ya kikafiri kwa ajili ya kulingania katika dini ya Allaah inajuzu ikiwa jambo hili lina taathira huko. Katika hali hiyo inajuzu. Hii ni safari ilio na maslahi.

Katika miji ya kikafiri wajinga wengi wamefanywa ni vipofu juu ya Uislamu. Hawajui lolote kuhusiana na Uislamu. Bali wamedhulumiwa. Wameambiwa kuwa Uislamu ni dini mbaya. Hili ni khaswa pale ambapo watu wa magharibini wanaposikia matendo haya yanayofanywa na wale wanaojiita kuwa ni waislamu. Hapo hupigwa na mshangao na husema “Uko wapi Uislamu?” Haya ni mambo mabaya. Hivyo matokeo yake waislamu wanafanya kuwakimbiza watu mbali na Uislamu kwa sababu ya matendo ya waislamu wenyewe. Tunamuomba Allaah atuongoze sote katika njia iliyonyooka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/25)
  • Imechapishwa: 16/01/2023