Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu makafiri:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi [wasimuone] Mola wao.”[1]

Watazuiliwa kutokamana na Allaah; hawatomuona. Kwa sababu wamemkufuru duniani na hivyo watazuiliwa kumuona siku ya Qiyaamah. Hapana shaka kwamba hii ni khasara na adhabu kubwa. Sambamba na hilo Aayah inathibitisha kuwa waumini si wenye kuzuiliwa kutokamana na Allaah siku ya Qiyaamah. Watamtazama kwa kumwangalia huko Aakhirah, kwa sababu wamemuamini duniani ilihali hawajamuona. Wamemuamini (Subhaanah) kwa alama na ujumbe Wake. Hivyo Allaah akawalipa kwa kuwatunuku kumuona siku ya Qiyaamah. Kutazama uso wa Allaah ndio neema kubwa zaidi ya Peponi. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hizi ni baadhi ya dalili zao kutoka ndani ya Qur-aan.

[1] 83:15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 75
  • Imechapishwa: 16/01/2023