Dalili nyingine Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameifasiri na kusema:

“Mazuri zaidi ni Pepo na ziada ni kutazama uso wa Allaah (´Azza wa Jall).”[2]

Allaah (Ta´ala) amesema:

لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ

“Watapata humo wayatakayo na Kwetu kuna zaidi.”[3]

Bi maana kuangalia uso mtukufu wa Allaah.

[1] 10:26

[2] Ahmad (4/332), Muslim (181) na at-Tirmidhiy (2558).

[3] 50:35

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 16/01/2023