Matembezi na matumizi kwa mama yangu wa kunyonya

Swali: Kuna mwanamke aliyeninyonyesha. Je, ana haki yeye na watoto wake juu yangu kuwatembelea?

Jibu: Kuhusu matembezi, anazingatiwa ni mama yako. Mtembelee. Kuhusu kumpa matumizi hulazimiki kumhudumia, lakini ukifanya hivo ni vyema. Kufanya hivo ni kwa njia ya kutenda wema na si kwa njia ya ulazima.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 309
  • Imechapishwa: 10/01/2025