Matatizo madogo, thawabu kidogo, na matatizo makubwa, thawabu nyingi

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس ـ رضي الله عنه ـ قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إذا أراد الله بعبده خيرا عجل له العقوبة في الدنيا، وإذا أراد بعبده الشر أمسك عنه بذنبه حتى يوافي به يوم القيامة))

43 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume  wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapompendelea mja wake kheri, basi humharakishia adhabu duniani, na akimtakia mja wake shari humzuilia dhambi zake ili amuadhibiwa kwazo siku ya Qiyaamah.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika malipo makubwa yanakuwa pamoja na mabalaa makubwa. Allaah (Ta´ala) anapowapenda watu, huwapa majaribio; yule anayeridhia basi hupata radhi [za Allaah], na yule mwenye kuchukia hupata khasira [za Allaah].”

Hadiyth ni nzuri

Matatizo mepesi yana malipo madogo. Matatizo mazito yana malipo makubwa. Allaah ni mwingi wa fadhilah kwa watu. Akiwapa mtihani kwa matatizo makubwa, basi anawalipa kwa ujira ulio mkubwa. Matatizo mepesi yana ujira mdogo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/259)
  • Imechapishwa: 12/03/2023