Uwajibu wa wazazi kuwachagulia watoto majina mazuri

Kwa hivyo inatakiwa kwa mtu awachagulie watoto wake majina mazuri ili aweze kupata ujira huo na awe amewatendea wema wavulana na wasichana wake. Ama kuleta majina mageni katika jamii, hili linaweza kuwaletea unyanyasikaji huko mbele na kila udhi analopata mtoto kwa sababu ya jina hili unakuwa ni mwenye kupata madhambi. Kwa sababu wewe mzazi ndiye uliyesababisha unyanyasaji wa jina hili la kigeni ambalo linalolengwa na kuwashangaza watu. Kwa ajili hii inatakiwa kwa mtu kuchagua majina mazuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/265)
  • Imechapishwa: 12/03/2023