Matangamano na Shiy´ah wanaowatukana Maswahabah

Swali: Ni upi wajibu wetu tukimsikia mmoja katika Shiy´ah anasema kuwa hawapendi Maswahabah na vilevile tumemsikia anawatukana Maswahabah ikiwa ni pamoja na mama wa waumini? Je, kutokana na kitendo hichi ni wajibu kutahadhari nao?

Jibu: Ndio, ni wajibu kutahadhari nao na kujitenga nao mbali kwa asiyekuwa na elimu. Ama ikiwa mtu ni katika wanachuoni na akawa na uwezo wa kujadiliana nao, afanye hivo huenda Allaah Akawaongoza. Ni wajibu ajadiliane nao na awawekee wazi yanayotolea dalili maandiko juu ya kuonesha fadhila za Maswahabah na fadhila za wamama wa waumini. Hili linahusu yule ambaye ni katika wanachuoni.

Kuhusiana na mtu ambaye sio katika wanachuoni, ajitenge nao mbali na awawafikishie wanachuoni ambao wanaweza kuwaraddi na kubainisha upotevu wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=13967
  • Imechapishwa: 17/11/2014