Anayewasifu na kuwapenda Ahl-ul-Bid´ah ni katika wao

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kupenda na kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah? Je, anaingia katika wao kwa tendo hilo?

Jibu: Ikiwa anawasifu Ahl-ul-Bid´ah, kama mfano wa Mu´tazilah, Ashaa´irah, Raafidhwah, Jahmiyyah, Khawaarij na Murji-ah, ndio anaingia katika wao. Kwa sababu ina maana anakubaliana nao. Mwenye kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah anakubaliana nao. Anawapenda Ahl-ul-Bid´ah na anachukia Sunnah. Hakuwasifu Ahl-ul-Bid´ah isipokuwa ni kwa sababu anachukia Sunnah na Ahl-us-Sunnah.

Ama ikiwa yuko na utata na hajui na ametatizwa, anatakiwa abainishiwe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=13967
  • Imechapishwa: 17/11/2014