Maswali kadhaa muhimu kuhusu Sutrah

Swali: Je, Sutrah ni lazima?

Jibu: Ni Sunnah iliyokokotezwa kwa anayeswali peke yake na imamu.

Swali: Wale watu aina tatu wanaoharibu swalah wanapopita mbele ya mswaliji[1] mtu anatakiwa kuanza upya?

Jibu: Ndio, mtu huyo akipita karibu na mswaliji au akapita baina ya mswaliji na Sutrah. Linamuhusu imamu na anayeswali peke yake. Kuhusu maamuma haiwadhuru. Mpitaji akipita mbele ya maamuma haiwadhuru kitu.

Swali: Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali pasi na Sutrah?

Jibu: Ndio.

Swali: Kwa hivyo katika hali hiyo ina maana kwamba mtu wakati mwingine aswali pasi na Sutrah?

Jibu: Ndio. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mwingine aliswali pasi na Sutrah.

Swali: Kwa hivyo mtu anaweza pia kuswali bila ya Sutrah?

Jibu: Pale ambapo atashindwa kupata Sutrah, ingawa bora ni kuswali mbele ya Sutrah.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya mtu muislamu inakatika kusipokuwa mbele yake mfano wa bakora ya anayepanda kipando: mwanamke, punda na mbwa mweusi.” (Muslim)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23015/حكم-السترة-للمصلي-وحكم-من-قطعت-صلاته
  • Imechapishwa: 15/10/2023