49. Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 4?

Swali 49: Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka huo?

Jibu: Katika mwezi wa Muharram, Abu Salamah aliongoza msafara wa kijeshi dhidi ya Banuu Asad.

Katika mwezi wa Safar, msafara wa kijeshi ulifanyika kwenye kisima cha Rajiy na msafara mwingine wa kijeshi uliongozwa na ‘Amr adh-Dhwamriy. Katika mwezi huohuo wakauliwa wanazuoni wa Maswahabah sabini kwa kuvizia na makabila ya Ri’, Dhakwaan na ´Uswayyah ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mwezi mzima akaomba du´aa dhidi ya wale waliowaua. Ndani ya mwezi huo ndipo Zayd bin Thaabit alijifunza Kiebrania.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 113
  • Imechapishwa: 15/10/2023