Maswali kadhaa muhimu kuhusu Sutrah na mbwa anayepita mbele ya mswaliji

Swali: Kuna mtu anaswali mbele yangu kisha nikamfanya kuwa Sutrah ambapo yeye anaswali na mimi pia naswali?

Jibu: Haidhuru. Jambo ni lenye wasaa.

Swali: Mwanamke Haram?

Jibu: Hadhuru. Mwanamke Haram hadhuru.

Swali: Mwanamke amepatwa na jini na wakati anaposwali anahisi kuwa mbwa anapita mbele yake na kadhalika?

Jibu: Akipita mbele yake ndani ya dhiraa tatu au akapita baina yake yeye na Sutrah yake basi aikate. Hapa ni pale ambapo mbwa huyo ni mweusi.

Swali: Je, airudie swalah yake?

Jibu: Airudie swalah akipita mbele ya mswaliji au baina yake yeye na Sutrah yake. Ni lazima kuiswali upya ikiwa ni swalah ya faradhi.

Swali: Shaykh umesema kuwa ikiwa ni swalah ya faradhi aikate swalah yake – vipi ikiwa ni swalah inayopendeza?

Jibu: Ataikata. Lakini hatolazimika kuirudia kwa sababu ni swalah inayopendeza. Akiirudia ni vyema na asipofanya hivo hatolazimika, kwa sababu ni swalah inayopendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23668/حكم-سترة-المصلي-وما-يقطع-الصلاة
  • Imechapishwa: 26/03/2024