Swali: Ibn-ul-Qayyim anaona kuwa inafaa kupokea zawadi ikiwa mashindano ni ya Qur-aan na Sunnah. Je, kunaingia pia mashindano ya utamaduni na adabu?

Jibu: Hapana. Hayakuwekwa katika Shari´ah. Adabu, mashairi na mfano wake ni mambo yameruhusiwa, lakini haifai kupokea tuzo katika vitu kama hivi. Tuzo zinachukuliwa katika vitu vilivyowekwa katika Shari´ah,  kama vile Fiqh, Qur-aan na Sunnah. Sarufi na kiarabu pia ni vitu vizuri, kwa sababu vinamsaidia mtu kuelewa Qur-aan na Sunnah. Kwa vile sarufi na kiarabu vinamsaidia mtu kuielewa Qur-aan na Sunnah, inafaa kuvichukulia tuzo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 12/03/2022