Swali: Ni yepi masharti ya Khutbah?
Jibu: Ni kwamba ndani yake kuwe na kumsifu Allaah, kumtukuza Allaah, kutamka shahaadah mbili, kuwakemea na kuwakumbusha watu. Baadhi ya wanazuoni wameweka sharti la kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi yao wameweka sharti la kusoma Aayah moja. Hivyo inafaa kufanya mambo haya: kumsifu Allaah na kumtukuza, kutamka shahaadah mbili, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaonya na kuwakumbusha watu.
Lengo ni kuwausia watu, kuwakumbusha, kuwafundisha, kuwaelekeza katika kheri na kuwaonya dhidi ya shari. Ikiwa atasoma Aayah moja au Aayah kadhaa wakati wa Khutbah, basi hili ni jambo jema. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Aayah katika Khutbah. Lakini wanazuoni wametofautiana kama ni sharti au si sharti? Wako waliolifanya kuwa sharti na wengine wamesema si sharti, lakini ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kusoma baadhi ya Aayah. Kwa kuwa akifanya hivyo atakuwa ametoka katika tofauti ya wale waliodai Khutbah haikamiliki bila ya kusoma Aayah.
Swali: Je, sifa na kumtukuza Allaah vinatakiwa katika Khutbah zote mbili?
Jibu: Ndio, katika Khutbah zote mbili.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31480/ما-شروط-خطبة-الجمعة
- Imechapishwa: 28/10/2025
Swali: Ni yepi masharti ya Khutbah?
Jibu: Ni kwamba ndani yake kuwe na kumsifu Allaah, kumtukuza Allaah, kutamka shahaadah mbili, kuwakemea na kuwakumbusha watu. Baadhi ya wanazuoni wameweka sharti la kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi yao wameweka sharti la kusoma Aayah moja. Hivyo inafaa kufanya mambo haya: kumsifu Allaah na kumtukuza, kutamka shahaadah mbili, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaonya na kuwakumbusha watu.
Lengo ni kuwausia watu, kuwakumbusha, kuwafundisha, kuwaelekeza katika kheri na kuwaonya dhidi ya shari. Ikiwa atasoma Aayah moja au Aayah kadhaa wakati wa Khutbah, basi hili ni jambo jema. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Aayah katika Khutbah. Lakini wanazuoni wametofautiana kama ni sharti au si sharti? Wako waliolifanya kuwa sharti na wengine wamesema si sharti, lakini ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kusoma baadhi ya Aayah. Kwa kuwa akifanya hivyo atakuwa ametoka katika tofauti ya wale waliodai Khutbah haikamiliki bila ya kusoma Aayah.
Swali: Je, sifa na kumtukuza Allaah vinatakiwa katika Khutbah zote mbili?
Jibu: Ndio, katika Khutbah zote mbili.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31480/ما-شروط-خطبة-الجمعة
Imechapishwa: 28/10/2025
https://firqatunnajia.com/masharti-ya-kusihi-kwa-ijumaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket