90 – Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf amenihadithia: “Nilimuuliza ´Aaishah, mama wa waumini: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anafungulia swalah yake kwa kitu gani anaposimama usiku?” Akasema: “Alikuwa anaposimama usiku huifungua swalah yake kwa:
اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَالَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَواتِ والأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادك فِيما كانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم
“Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl! Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ambaye ni Mjuzi wa mambo yenye kujificha na yalio ya wazi! [Siku moja] utahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana! Niongoze mimi katika haki katika yale waliotafautiana kwa idhini Yako, kwani hakika Wewe unamuongoza umtakaye katika njia ilionyoka.”[1]
Ameipoke Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna kufanya Tawassul kwa Allaah (Ta´ala) kutokana na uola wa Malaika hawa watatu: Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl. Hilo ni kwa sababu Malaika hawa watatu wamepewa kazi kwa yale yanayofanya kuwepo kwa uhai. Jibriyl amepewa kazi ya Wahy, kitu ambacho hufanya mioyo na roho zikapata uhai. Mikaaiyl amepewa kazi ya kuteremsha mvua, ambayo ndio hufanya viumbe kama vile wana wa Aadam, wanyama na mimea kupata uhai. Israafiyl amepewa kazi ya kupuliza baragumu, jambo ambalo litafanya roho kurudi kwenye viwiliwili vyake na hivyo watu watoke ndani ya makaburi yao wakiwa hai.
[1] Muslim (770).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 93-94
- Imechapishwa: 29/10/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 93-94
Imechapishwa: 29/10/2025
https://firqatunnajia.com/25-duaa-ya-kufungulia-swalah-ya-usiku/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket