Swali: Je, kufichika na kuonekana uwazi wa mambo hubadilika kulingana na zama na maeneo?
Jibu: Hababadiliki. Kadiri ujinga unavyoongezeka, ndivyo tatizo linavyokuwa kubwa zaidi. Kadiri Uislamu unavyokuwa mgeni zaidi, ndivyo hali inavyokuwa nzito zaidi. Lakini mradi mtu yuko miongoni mwa waislamu, anasikia Qur-aan na anasikia Sunnah, basi Ujumbe umemfikia. Allaah amesema:
هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ
“Hii ni ufikishwaji wa ujumbe kwa watu na ili wawaonye kwayo.”[1]
Qur-aan imefika. Amesema tena (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ
“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[2]
Ameshafikiwa na Qur-aan, lakini unapomwita njoo tufanye hivi, anakubishia, anapigana nawe na hakubali kufaidika. Waabudu makaburi hivi sasa ni vigumu sana kuelewana nao katika masuala ya kumwabudu Allaah pekee isipokuwa kwa ukali. Hawataki yeyote awaeleze; wanadhani wako katika haki, isipokuwa wale ambao Allaah amewarehemu. Tunamuomba Allaah atupe salama.
Swali: Mazungumzo haya ni kuhusu Tawhiyd pekee au hata katika masuala ya Bid´ah zinazofikisha kiwango cha ukafiri kama za Jahmiyyah?
Jibu: Masuala ambayo hayafikii ukafiri ni jambo jepesi. Tunachokusudia ni yale masuala yanayofikisha kwenye ukafiri.
Swali: Hukumu inatolewa kwa ujumla kwa watu wa kawaida au kunahitaji upambanuzi?
Jibu: Watu wa kawaida wakiwa wanaamini dini ya viongozi wao, basi wanahesabiwa pamoja nao. Ni kama walivyo watu wa kawaida wa mayahudi na manaswara – wao pia ni miongoni mwao. Ama jambo ambalo linaweza kufichika, kama uwezo wa jumla wa Allaah, mfano wa yule mtu aliyewaamrisha jamaa zake wamchome moto huku akadhani kuwa akichomwa na majivu yake yakitawanywa katika siku yenye joto kali hatapatikana tena na hivyo ataokoka, basi Allaah akaamrisha ardhi na bahari zikusanye vilivyomo, kisha akamwambia: ”Ni nini kilichokufanya ufanye hivi?” Akasema: ”Khofu Yako, ee Mola wangu.” Matokeo yake Allaah akamsamehe.
[1] 14:52
[2] 6:19
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31466/هل-يتغير-العذر-بالجهل-باختلاف-الازمنة-والامكنة
- Imechapishwa: 28/10/2025
Swali: Je, kufichika na kuonekana uwazi wa mambo hubadilika kulingana na zama na maeneo?
Jibu: Hababadiliki. Kadiri ujinga unavyoongezeka, ndivyo tatizo linavyokuwa kubwa zaidi. Kadiri Uislamu unavyokuwa mgeni zaidi, ndivyo hali inavyokuwa nzito zaidi. Lakini mradi mtu yuko miongoni mwa waislamu, anasikia Qur-aan na anasikia Sunnah, basi Ujumbe umemfikia. Allaah amesema:
هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ
“Hii ni ufikishwaji wa ujumbe kwa watu na ili wawaonye kwayo.”[1]
Qur-aan imefika. Amesema tena (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ
“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[2]
Ameshafikiwa na Qur-aan, lakini unapomwita njoo tufanye hivi, anakubishia, anapigana nawe na hakubali kufaidika. Waabudu makaburi hivi sasa ni vigumu sana kuelewana nao katika masuala ya kumwabudu Allaah pekee isipokuwa kwa ukali. Hawataki yeyote awaeleze; wanadhani wako katika haki, isipokuwa wale ambao Allaah amewarehemu. Tunamuomba Allaah atupe salama.
Swali: Mazungumzo haya ni kuhusu Tawhiyd pekee au hata katika masuala ya Bid´ah zinazofikisha kiwango cha ukafiri kama za Jahmiyyah?
Jibu: Masuala ambayo hayafikii ukafiri ni jambo jepesi. Tunachokusudia ni yale masuala yanayofikisha kwenye ukafiri.
Swali: Hukumu inatolewa kwa ujumla kwa watu wa kawaida au kunahitaji upambanuzi?
Jibu: Watu wa kawaida wakiwa wanaamini dini ya viongozi wao, basi wanahesabiwa pamoja nao. Ni kama walivyo watu wa kawaida wa mayahudi na manaswara – wao pia ni miongoni mwao. Ama jambo ambalo linaweza kufichika, kama uwezo wa jumla wa Allaah, mfano wa yule mtu aliyewaamrisha jamaa zake wamchome moto huku akadhani kuwa akichomwa na majivu yake yakitawanywa katika siku yenye joto kali hatapatikana tena na hivyo ataokoka, basi Allaah akaamrisha ardhi na bahari zikusanye vilivyomo, kisha akamwambia: ”Ni nini kilichokufanya ufanye hivi?” Akasema: ”Khofu Yako, ee Mola wangu.” Matokeo yake Allaah akamsamehe.
[1] 14:52
[2] 6:19
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31466/هل-يتغير-العذر-بالجهل-باختلاف-الازمنة-والامكنة
Imechapishwa: 28/10/2025
https://firqatunnajia.com/kupewa-udhuru-kwa-ujinga-kunatokana-na-zama-na-maeneo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket