Marafiki zake wanakataa kumpa picha azichome baada ya kutubia

Swali: Mimi nina baadhi ya picha kwa marafiki zangu na nimewaomba picha hizo ili niziharibu kwa kuogopa adhabu ya Allaah. Baadhi yao wamenipa na wengine wamenikataa kwa hoja kwamba dhambi ni kwao na mimi sipati kitu. Je, hayo ni kweli?

Jibu: Tawbah ya kweli kutokamana na madhambi Allaah anayafuta kwayo madhambi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

َتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.” (24:31)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na tawbah inafuta yaliyokuwa kabla yake.”

Ni lazima kwako kuharibu picha ulizonazo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha yoyote isipokuwa uiharibu wala kaburi lililonyanyuliwa isipokuwa umelisawazisha.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Kuhusu picha zilizo kwa watu wengine ukiwaomba nazo na wakakukatalia kukupa nazo basi dhimma yako imetakasika na zimeenea na tawbah. Madhambi ziko kwa wale wenye kuzihifadhi. Allaah atutengeneze sote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/422) https://binbaz.org.sa/fatwas/940/%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%88%D8%A8%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B5%D9%88%D8%AD-%D9%8A%D9%85%D8%AD%D9%88-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87-%D8%A8%D9%87%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%86%D9%88%D8%A8
  • Imechapishwa: 31/01/2020