Watu wenye busara miongoni mwa Waislamu wanatambua hili. Kufanya uasi, kuwalea watu katika mapinduzi na kuwahujumu, ni jambo linaudhuru Uislamu na Waislamu.

Mmepata mafunzo Somali, Yemen, ´Iraaq, Algeria na leo mmepata mafunzo katika kila nchi ambapo kumepitika uasi. Hakuna kinachopelekea katika uasi huu isipokuwa kufanya Uislamu na Waislamu kuwa dhaifu, umwagikaji wa damu, ukiukwaji wa heshima [za watu], kuangamiza mali na uharibifu. Baada ya haya yanatosheleza peke yake kwa mtu mwenye akili kushikamana barabara na manhaj Salaf-us-Swaalih na kwamba ndio haki na ndio yenye kutokamana kimatendo na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume. Hivyo asapoti maandiko haya, akili na uzowefu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/131)
  • Imechapishwa: 19/05/2015