Wakati eda ya ´Aatikah ilipomalizika, az-Zubayr bin al-‘Awwaam alimposa. Akamwambia:

“Ndio, ikiwa unakubali masharti yangu matatu[1] niliyomuwekea ´Umar.”

Akayakubali na kumuoa. Alipotaka kutoka kwenda kuswali ´Ishaa, az-Zubayr akafadhalika. Akaliona hilo na kusema:

“Unataka kunizuia?”

Usiku mmoja subira yake az-Zubayr ikafika mwisho. Alipotoka kwenda ‘Ishaa’ az-Zubayr alikuwa ameshamtangulia na akakaa katika njia kwa namna ya kwamba hakuweza kumuona. Alipompita akasimama na kumshika kwenye makalio yake. Kwa hofu, akaondoka haraka. Usiku uliofuata alisikia adhaana na hakutikisika. az-Zubayr alipoona kwamba hakutikisika, akamwambia:

“Una nini? Adhaana hiyo.” Akasema: “Watu wameharibika.”

Hakutoka tena baada ya hapo. Aliendelea kuolewa na az-Zubayr hadi hapo az-Zubayr alipouliwa katika vita vya ngamia.

[1] “Usinipige, usinizuie kutokana na haki na usinizuie na ‘Ishaa’ ya baadaye katika msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).” (at-Tamhiyd (23/406)

  • Mhusika: Imaam Abu ´Umar Yuusuf bin ´Abdil-Barr al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tamhiyd (23/406-407)
  • Imechapishwa: 29/09/2023