Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu kuhusu Ahl-ul-Fatrah na wale ambao hawakufikiwa na ulinganizi na watoto wa washirikina waliofariki?

Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba watasimamishiwa hoja siku ya Qiyaamah. Haya yametajwa na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) na yametajwa pia na Ibn Kathiyr na wengineo katika mnasaba wa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.”[1]

[1] 17:15

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25064/ما-الراجح-في-اصحاب-الفترة-ومن-لم-تبلغه-الدعوة
  • Imechapishwa: 10/02/2025