Swali: Vipi tunatofautisha kati ya miujiza na karama?
Jibu: Msingi ni kwamba ni kitu kimoja. Karama na miujiza ni mambo yanayoenda kinyume na mazoea ya kawaida. Ikiwa jambo hilo linatokea kwa njia ya changamoto, kama vile ilivyokuwa kwa Mitume, hili kwa mujibuwa istilahi huitwa ”miujiza” na pia linaweza kuitwa ”karama” kwa maana ya jumla. Na ikiwa jambo hilo linatokea kupitia waumini wa kawaida ambao si Mitume wala hawadai utume, bali ni miongoni mwa wafuasi wa Mitume, basi hii inajulikana zaidi kama ”karama”. Hata hivyo karama hizi pia ni muujiza kwa Mtume aliyekuja na dini ambayo muumini huyo anaifuata. Lakini ikiwa jambo hilo halihusiani na Mitume wala waumini, basi ni miongoni mwa uchawi unaoletwa na mashaytwaan, ingawa linaweza kuitwa kuwa ni jambo lsiilo la kawaida. Uhakika wa mambo ni uchawi, urembeshaji na udanganyifu kutoka kwa mashaytwaan ili watu waone kuwa jambo hilo limetoka kwa muumini au Mtume, hali si hivyo. Kwa sababu hiyo, wanazuoni wamesema, kama ilivyotangulia mizani ya kutofautisha ni utekelezaji wa Shari´ah. Mtu anayefuata Shari´ah na amesimama sawa juu yake kwa nje na kwa ndani, basi jambo lolote lisilo la kwaida litakalomtokea ni karama. Lakini ikiwa si mwenye kushikamana na dini, basi mambo hayo yasiyo ya kwaida yanatoka kwa mashaytwaan kwa ajili ya kuwapotosha watu au kutimiza matakwa ya wapenzi wao miongoni mwa watu, kama vile wanavyofanya wachawi, waganga wa kienyeji na wanajimu. Haya yote ni kwa sababu ya udanganyifu wa mashaytwaan na hadaa kwa watu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25111/ما-الفرق-بين-المعجزات-والكرامات
- Imechapishwa: 10/02/2025
Swali: Vipi tunatofautisha kati ya miujiza na karama?
Jibu: Msingi ni kwamba ni kitu kimoja. Karama na miujiza ni mambo yanayoenda kinyume na mazoea ya kawaida. Ikiwa jambo hilo linatokea kwa njia ya changamoto, kama vile ilivyokuwa kwa Mitume, hili kwa mujibuwa istilahi huitwa ”miujiza” na pia linaweza kuitwa ”karama” kwa maana ya jumla. Na ikiwa jambo hilo linatokea kupitia waumini wa kawaida ambao si Mitume wala hawadai utume, bali ni miongoni mwa wafuasi wa Mitume, basi hii inajulikana zaidi kama ”karama”. Hata hivyo karama hizi pia ni muujiza kwa Mtume aliyekuja na dini ambayo muumini huyo anaifuata. Lakini ikiwa jambo hilo halihusiani na Mitume wala waumini, basi ni miongoni mwa uchawi unaoletwa na mashaytwaan, ingawa linaweza kuitwa kuwa ni jambo lsiilo la kawaida. Uhakika wa mambo ni uchawi, urembeshaji na udanganyifu kutoka kwa mashaytwaan ili watu waone kuwa jambo hilo limetoka kwa muumini au Mtume, hali si hivyo. Kwa sababu hiyo, wanazuoni wamesema, kama ilivyotangulia mizani ya kutofautisha ni utekelezaji wa Shari´ah. Mtu anayefuata Shari´ah na amesimama sawa juu yake kwa nje na kwa ndani, basi jambo lolote lisilo la kwaida litakalomtokea ni karama. Lakini ikiwa si mwenye kushikamana na dini, basi mambo hayo yasiyo ya kwaida yanatoka kwa mashaytwaan kwa ajili ya kuwapotosha watu au kutimiza matakwa ya wapenzi wao miongoni mwa watu, kama vile wanavyofanya wachawi, waganga wa kienyeji na wanajimu. Haya yote ni kwa sababu ya udanganyifu wa mashaytwaan na hadaa kwa watu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25111/ما-الفرق-بين-المعجزات-والكرامات
Imechapishwa: 10/02/2025
https://firqatunnajia.com/tofauti-kati-ya-miujiza-na-karama/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)