Maoni ya wanazuoni wengi kuhusu mapigano miezi mitukufu

Swali: Maneno yake:

“Kama heshima ya mwezi wenu huu.”

ndani yake kuna ushahidi kwa wale waliosema kwamba hukumu ya kupigana vita miezi mitakatifu haijafutwa?

Jibu: Ndani yake kuna hoja kwa wale miongoni mwa wanazuoni waliosema kwamba miezi mitakatifu bado ipo; nayo ni Muharram, Dhul-Qa’dah, Dhul-Hijjah – mitatu – na ya nne ni Rajab mmoja uliojitenga peke yake. Hii minne, kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, wanaona kwamba mapigano ndani yake yamefutwa na kwamba hakuna ubaya. Lakini baadhi ya wanazuoni wameona kuwa bado ipo. Allaah amesema:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ

”Wanakuuliza kuhusu kupigana ndani ya mwezi mtukufu. Sema: “Kupigana ndani yake ni dhambi kubwa.”[1]

[1] 02:217

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25016/ما-صحة-القول-بنسخ-القتال-في-الاشهر-الحرم
  • Imechapishwa: 25/01/2025