Amekosa Hajj kisha akatoka kwenye Ihraam kwa kufanya ´Umrah

Swali: Ikiwa atakosa Hajj kisha akatoka kwenye Ihraam kwa kufanya ‘Umrah – Je, haifanani na aliyenuia kuhiji kwa Tamattu‘?

Jibu: Hili ndilo alilolitoa fatwa ´Umar. Aliwajibisha juu yao hajj inayofuata na pia kutoa fidia na aliwafananisha na aliyenuia kufanya ‘Umrah na Hajj kwa pamoja, au aliyenuia Hajj peke yake kisha akatoka kwenye Ihraam kwa kufanya ‘Umrah. Aliwafananisha nao kwa sababu anahiji na kutoa kuchinja kichinjwa, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowaongoza Maswahabah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25034/ما-حكم-من-فاته-الحج-ثم-تحلل-بعمرة
  • Imechapishwa: 25/01/2025