01 – Sharti ya kwanza ya shaahadah – Utambuzi

Sharti ya kwanza ni utambuzi.

Maana yake ni utambuzi wa maana yake na kutambua makusudio yake hali ya kukanusha na kuthibitisha ambayo inayopingana na ujinga wa shahaadah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ

“Basi elewa kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”[1]

وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Na wala hawana uwezo wa kumiliki uombezi wale wanaowaomba badala Yake isipokuwa aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua.”[2]

Bi maana ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Je, mnatumai kuwa watakuaminini na hali lilikuwa kundi katika wao linasikia maneno ya Allaah kisha linayapotosha baada ya kuyaelewa na hali wanajua?”[3]

Bi maana nyoyo zao zilitambua yale yanayotamkwa na ndimi zao. Allaah (Ta´ala) amesema tena:

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

“Allaah ameshuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Malaika na wenye elimu [pia wameshuhudia], ni Mwenye kusimamisha kwa uadilifu. Hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima.”[4]

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ

“Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika hapana vyenginevyo wanakumbuka wenye akili tu.”[5]

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si vyenginevyo wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”[6]

وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ

”Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye elimu.”[7]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kufa na huku akitambua ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, ataingia Peponi.”[8]

[1] 47:19

[2] 43:86

[3] 2:75

[4] 3:18

[5] 39:9

[6] 35:28

[7] 29:43

[8] Ahmad (1/65).

  • Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/334)
  • Imechapishwa: 26/01/2025