Sharti ya pili ni yakini.
Yakini ambayo inapingana na shaka. Maana yake ni kwamba mwenye kuitamka shahaadah awe na yakini ya kukata kabisa juu ya majulisho ya neno hili. Imani haina maana yoyote ikiwa inatokana na dhana badala ya yakini. Mtu aseme nini ikiingiwa na shaka? Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ
”Hakika hapana vyengine waumini ni wale waliomwamini Allaah na Mtume Wake kisha wakawa si wenye shaka na wanapambana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah. Hao ndio wakweli.”[1]
Akashurutisha ukweli wa kumuamini kwao Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wawe si wenye kusita, nako ni kutotia shaka. Kuhusu anayetia shaka, huyo ni katika wanafiki – ulinzi unaombwa kutoka kwa Allaah – ambao Allaah amesema juu yao:
إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ
“Hakika hapana vyengine wanaokuomba ruhusa ni wale ambao hawamuamini Allaah na siku ya Mwisho na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita.”[2]
Imethibiti kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah. Hakuna mja yeyote anayekutana Allaah akiwa na [shahaadah] mbili hizi, isipokuwa ataingia Peponi.”[3]
Hapa ameshurutisha ili mwenye kutamka shahaadah aweze kuingia Peponi iwe moyo wake unayakinisha na asiwe na si mwenye kuitilia shaka. Shaka ikiondoka, basi kunaondoka kile kilichotiliwa sharti.
[1] 49:15
[2] 9:45
[3] Muslim (01/55-57) .
- Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/334-335)
- Imechapishwa: 26/01/2025

Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/334-335)
Imechapishwa: 26/01/2025
https://firqatunnajia.com/02-sharti-ya-pili-ya-shaahadah-yakini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)