Sharti ya tatu ni kuyakubali kwa moyo na ulimi wake yale yanayopelekea katika shahaadah. Allaah (´Azza wa Jall) ametusimulia namna alivyowaokoa wale walioikubali shahaadah na kuwaadhibu wale wenye kuirudisha na kuikataa. Amesema (Ta´ala):
وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
“Hivyo ndivyo hatukutuma kabla yako katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake walisema: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao. Akasema: “Japo hata kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mmewakuta nao baba zenu?” Wakasema: “Hakika sisi tunayakanusha yale mliyotumwa nayo. Basi tukawalipizi kisasi. Hebu tazama vipi ulikuwa mwisho wa wenye kukadhibisha!”[1]
ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ
“Kisha Tunawaokoa Mitume wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu kuwaokoa waumini.”[2]
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ
“Kwa hakika Tuliwatuma kabla yako Mitume kwa watu wao wakawajia kwa hoja za wazi, tukawalipiza wale ambao wamefanya uhalifu; na ni haki daima Kwetu kuwanusuru waumini.”[3]
Vilevile ametueleza zile thawabu alizowapa wale walioikubali shahaadah kama alivyotueleza pia adhabu aliyowaandalia wale walioikataa. Amesema (Ta´ala):
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ
“Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Allaah, na waongozeni kwenye njia ya Moto uwakao vikali. Wasimamisheni, hakika wao watahojiwa… ”[4]
Mpaka alipofikia (´Azza wa Jall) kusema:
إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ
“Hakika wao walipokuwa wakiambiwa “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” wanafanya kiburi na wanasema: “Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”[5]
Allaah (Ta´ala) akafanya sababu ya kuadhibiwa kwayo ni kule kufanya kwao kiburi kutamka “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na kumkadhibisha yule ambaye amekuja na shahaadah hiyo. Hawakukanusha yale yaliyokanushwa na shaahadah na wala hawakuthibitisha yale yaliyothibitishwa na shahaadah hiyo. Bali walisema hali ya kupinga na kufanya kiburi:
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ
“Amewafanya miungu wote hawa kuwa mungu Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno! Na wakaondoka wakuu miongoni mwao [wakisema]: “Nendeni na subirini juu ya miungu yenu, hakika hili ni jambo linalotakwa. Hatukusikia haya katika dini ya mwisho, haya si chochote isipokuwa ni jambo lilozushwa tu.””[6]
Walisema:
أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ
“Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”
Ndipo Allaah akawakadhibisha na kuwaraddi na akasema kuhusu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ
”Bali amekuja kwa haki na amewasadikisha Mitume.”[7]
Kisha akasema kuhusu wale wenye kuikubali shahaadah:
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
“Isipokuwa waja wa Allaah wanaomtakasia nia Allaah – hao watapata riziki maalum: matunda – nao ni wenye kukirimiwa: katika mabustani yenye neema.”[8]
[1] 43:23-25
[2] 10:103
[3] 30:47
[4] 37:22-24
[5] 37:35
[6] 38:5-7
[7] 37:37
[8] 37:40-43
- Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/335-336)
- Imechapishwa: 26/01/2025

Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/335-336)
Imechapishwa: 26/01/2025
https://firqatunnajia.com/03-sharti-ya-tatu-ya-shaahadah-kuikubali/