Ibn Baaz kuhusu kuchinja Ramadhaan kwa ajili ya wazazi wawili II

Swali: Katika Ramadhaan kile hufanywa na baadhi ya watu kinachoitwa “Chakula cha  wazazi” ambapo kunachinjwa baadhi ya kondoo na kuwapa masikini na wahitaji?

Jibu: Ni swadaqah, hapana vibaya na kizuizi. Ni swadaqah katika Ramadhaan. Inapokuja Ramadhaan huongezeka thawabu zake. Hivyo ikiwa atachinja na kugawa hiyo kwa masikini, kwa niaba yake mwenyewe, watu wa nyumbani kwake au wote wao hali ya kutafuta fadhilah za Ramadhaan au siku kumi za Dhul-Hijjah, hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25037/حكم-ما-يسمى-بعشاء-الوالدين
  • Imechapishwa: 26/01/2025