Swali: Je, kuswali kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Dhuhaa akiwa Makkah hali ya kuwa ni msafiri kunafahamisha kwamba swalah za Sunnah zinaweza kuswaliwa bila kizuizi safarini?

Jibu: Muislamu ni mfuataji, si mzushi. Muislamu anapaswa kufuata na kuiga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Dhuhaa, nasi twaswali Dhuhaa. Aliswali Witr usiku, nasi twaswali Witr usiku. Aliswali Tahajjud usiku akiwa safarini, nasi twaswali Tahajjud safarini. Aliacha Sunnah ya Dhuhr, Maghrib na ´Ishaa nasi tunaacha. Aliswali Raatibah ya Fajr, nasi tunaiswali safarini. Sisi ni wafuataji. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah.”[1]

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah.”[2]

Alichofanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) twafanya na alichoacha tunaacha. Hiyo ndiyo Sunnah.

[1] 03:31

[2] 33:21

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25041/هل-يجوز-صلاة-النافلة-في-السفر
  • Imechapishwa: 26/01/2025