Inafaa kuchinja Hadiy ya Tamattu´ Muzdalifah?

Swali: Vipi ikiwa kichinjwa cha Hadiy ya Tamattu´ katika Minaa kuna msongamano na mtu akatoka hadi Muzdalifah na kuchinja?

Jibu: Eneo lote la Haram linaruhusiwa kuchinja. Minaa ni bora zaidi. Hapana vibaya ikiwa mtu atachinja Makkah au Muzdalifah. Jambo lenye wasaa. Iwapo mtu ataingia Makkah na kuchinja ndani ya Makkah ni vyema. Jambo lenye wasaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25042/هل-يجوز-ذبح-هدي-التمتع-في-مزدلفة
  • Imechapishwa: 26/01/2025