Ambaye amekatikiwa ilihali kishafanya hajj ya kwanza

Swali: Kipi kinachomlazimu mtu ambaye ameishiliwa ikiwa amekwishahii hajj ya faradhi?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu. Aendelee tu. Ikiwezekana kwake kuendelea, basi aendelee. Ikiwa haiwezekani, basi atachinja, atanyoa au kufupisha nywele na kutoka kwenye Ihraam. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoishiliwa hawakuambiwa kuwa wanalazimika kufanya ´Umrah peke yake. Bali aliwaamuru wachinje, wanyoe au wafupishe na watoke kwenye Ihraam. Halafu akafanya ‘Umrah mwaka uliofuata. Aliita ´Umrah ya kulipa´, lakini hakumlazimisha yeyote kati ya watu kuilipa. Aliifanya ‘Umrah na wale walioweza kuifanya. Haijathibitika kwamba alimuwajibisha yeyote kuilipa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25032/ماذا-يجب-على-المحصر-اذا-كان-قد-حج-الفريضة
  • Imechapishwa: 25/01/2025