Swali: Ni ipi hukumu wanawake kuyatembelea makaburi?

Jibu: Kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa haifai kwa wanawake kuyatembelea makaburi. Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tumekatazwa kufuata jeneza na wala hatukutiliwa mkazo.”

Imekuja katika Hadiyth nyingine:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi, wenye kujenga misikiti juu yake na wenye kuyaweka mataa.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-زيارة-النساء-للقبور
  • Imechapishwa: 12/06/2022