01. Vifaa vipya, ulinganizi uleule

Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah. Tunamhimidi Yeye, tunamwomba msaada, msamaha na kutubia Kwake. Tunajilinda kwa Allaah kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yeyote anayeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha, na yeyote anayepotoshwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake – swalah na amani ziwe juu yake yeye, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Amma ba´d:

Kumezungumzwa sana kuhusu njia za kulingania na kama zimejengeka juu ya Qur-aan na Sunnah na hivyo ulinganizi hautakiwi kuzidisha juu yake zaidi ya yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, au ni jambo la Ijtihaad ambalo mlinganizi ana uamuzi wa kuzidisha kile atakachoona kinafaa kwa wakati na mahali ili aweze kufikia lile lengo la wakati huo. Pale ilipokuwa maoni yanayosema kuwa njia ya ulinganizi ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ndio maoni ya haki na inayosapotiwa kwa hoja za ki-Shari´ah, ndipo nikamuomba Allaah msaada wa kuandika kitabu hiki kwa ajili ya kuinusuru haki na kuwatakia mema viumbe. Sambamba na hilo nimeegemea juu ya Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf. Humo nimebainisha kwamba vifaa vya kisasa na zana zingine hazipingani na kule ulinganizi kuhitajia Qur-aan na Sunnah, kwa sharti zana hizo za kisasa zisiwe zimekatazwa kwa mtazamo wa ki-Shari´ah. Nimebainisha vilevile  ya kwamba njia za ulinganizi zinatosha kabisa kueneza ulinganizi kwa njia timilifu na kamili, pasi na kujali zama na mahali. Aidha nimezindua kuwa maoni yanayosema kuwa njia za ulinganizi hazikujengeka juu ya Qur-aan na Sunnah ni moja katika misingi inayopotosha katika dini.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 28/07/2022