Swali: Ni ipi hukumu ya tamko:

”Allaah anaulizia hali yako?”

Jibu: Ibara hiyo haijuzu. Kwa sababu inampa mtu dhana ya kwamba Allaah (Ta´ala) hajui jambo hilo na hivyo anahitaji kuuliza. Inatambulika kuwa jambo hilo ni khatari. Ukweli ni kwamba msemaji hakusudii hivo. Hakusudii kuwa kuna jambo linalofichikana kwa Allaah na hivyo ndio akahitaji kuuliza. Lakini ibara hiyo inaweza kufidisha maana hiyo na kumfanya mtu akafahamu kimakosa maana hiyo. Kwa hiyo ni lazima kujiepusha nayo na ayabadilishe kwa kusema:

“Namuomba Allaah akusherekeeni.”

“Namuomba Allaah akufanyie upole.”

na mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 01/07/2022