Swali: Kuhusiana na kuwauza mbwa waliyopewa mafunzo, wako baadhi ya wanafunzi wanaosema kuwa kinachofaa ni ile thamani ya mafunzo na sio mbwa mwenyewe…
Jibu: Hizi ni hila. Ni hila na haisilihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza biashara ya mbwa. Kisha anakuja mtu na kusema kuwa ni halali na kwamba ni thamani ya mafunzo ndio yenye kuuzwa? Sio thamani ya mafunzo kabisa inayouzwa, ni mbwa mwenyewe. Imekuja katika Hadiyth:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza thamani ya mbwa… ”[1]
Iko wazi.
[1] al-Bukhaariy (2237).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
- Imechapishwa: 09/12/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)