Mambo ya kufanya kwa aliyekasirika

Swali: Nini mtu anatakiwa kufanya wakati anapokasirika?

Jibu: Aseme:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

“Najilinda kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”

Atawadhe ikimsahilikia kutawadha.

Aketi chini akiwa amesimama.

Anyamaze akiwa anazungumza.

Afanye hayo mpaka pale itakapotulia hasira yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22372/ما-المشروع-فعله-عند-الغضب
  • Imechapishwa: 10/03/2023