Mama anataka mke wangu aoneshe uso mbele ya ndugu zangu wa kiume

Swali: Mamangu bado ni mwenye kuendelea kumuomba mke wangu kuonesha uso wake mbele ya ndugu zangu ambao wamekwishabaleghe. Nimeshamnasihi mara nyingi ya kwamba hili halijuzu, lakini bado ameng´anga´ania kumuomba hili mke wangu. Unaninasihi nini katika jambo hili?

Jibu: Tunakunasihi kumuasi katika jambo hili. Haijuzu kwenu kumtii katika kumuasi Allaah (´Azza wa Jall).

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Kiumbe yeyote yule. Hata baba hatiiwi katika kumuasi Allaah (´Azza wa Jall):

وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا

“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii.” (29:08)

Haijuzu kumtii mzazi katika kumuasi Allaah (´Azza wa Jall), si mzazi wala mwengine yeyote.

Check Also

Baba anampiga msichana anamtishia maisha

Swali: Baba yangu anazungumza na mimi kwa ukali, ananipiga na ananitishia kuniua ambapo mume wangu …