Mama anamuomba pesa kuwapa ndugu zake wasiotaka kufanya kazi

Swali: Kuna mtu ambaye mama yake anamuomba pesa ili awape watoto wake wakubwa na hivyo awasaidie juu ya kubweteka na kutofanya kazi. Je, ampe pesa akimuomba kwa lengo hilo?

Jibu: Ikiwa mambo ni hivyo anachukua pesa kwako na kuwapa ndugu zako, haijuzu kwake kufanya hivo. Lakini yeye anatakiwa kumpa ili kumridhisha. Lakini yeye kuzitumia kwa njia isiyostahiki, yeye ndiye mwenye kubeba jukumu hilo. Lakini yeye muda wa kuwa ana uwezo ampe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (03)
  • Imechapishwa: 22/02/2024