Swali: Je, kumnyamazisha ambaye anawasengenya watu ni katika kuamrisha mema na kukemea maovu?

Jibu: Ndio, ni aina kubwa za kukemea maovu. Ambaye anawasengenya watu mnasihi, mtahadharishe na mukhofishe juu ya Allaah (´Azza wa Jall). Usinyamaze na wala usikae naye. Bali unapaswa kumnasihi na ujaribu kumzuia kusengenya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (03)
  • Imechapishwa: 22/02/2024