Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua malipo kwa ajili ya kuadhini?
Jibu: Haijuzu kuchukua malipo kwa ajili ya kuadhini kwa sababu ni ´ibaadah miongoni mwa ´ibaadah zingine. Haijuzu kuchukua malipo kwa ajili ya kufanya ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ
”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake, basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo; [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”[1]
Jengine ni kwamba akikusudia dunia kwa ajili ya adhaana yake inakuwa batili na haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[2]
Hata hivyo inafaa kupokea mshahara kwa ajili ya kutoa adhaana. Kulipa mishahara ni jambo linafanywa kwa ajili ya manufaa ya waislamu na kutoa adhaana ni miongoni mwa manufaa ya waislamu.
[1] 11:15-16
[2] Muslim (1718).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/163-164)
- Imechapishwa: 07/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua malipo kwa ajili ya kuadhini?
Jibu: Haijuzu kuchukua malipo kwa ajili ya kuadhini kwa sababu ni ´ibaadah miongoni mwa ´ibaadah zingine. Haijuzu kuchukua malipo kwa ajili ya kufanya ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ
”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake, basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo; [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”[1]
Jengine ni kwamba akikusudia dunia kwa ajili ya adhaana yake inakuwa batili na haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[2]
Hata hivyo inafaa kupokea mshahara kwa ajili ya kutoa adhaana. Kulipa mishahara ni jambo linafanywa kwa ajili ya manufaa ya waislamu na kutoa adhaana ni miongoni mwa manufaa ya waislamu.
[1] 11:15-16
[2] Muslim (1718).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/163-164)
Imechapishwa: 07/07/2026
https://firqatunnajia.com/malipo-kwa-ajili-ya-kuadhini/