Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Aidha wanapoona namna ambavyo maimamu waliafikiana katika kumsema vibaya Mariysiyyah, wengi wao walimkufurisha au wakampita upotofuni na kwamba yale yanayosemwa na hawa waliokuja nyuma ndio yaleyale yaliyosemwa na Mariysiyyah, basi utabainika uongofu kwa yule ambaye Allaah anataka kumwongoza. Hata hivyo makusudio ya fatwa hii sio kuingia kina ndani mada hii, nitaashiria kanuni za mambo peke yake. Mwenye busara ataangalia na kutafiti mwenyewe.
MAELEZO
Baadhi ya wanazuoni waliwakufurisha Jahmiyyah kwa sababu ya imani yao ya ukafiri na upotofu. Baadhi yao hawakuwakufurisha wale wanaowafuata kichwa mchunga, lakini waliwahukumu kuwa wamepotea. Ama yule anayekuwa mwanachuoni miongoni mwao na anakusudia kuwapotosha watu, basi huyo ni kafiri bila shaka. Kwa sababu ni mwenye kufanyia inadi Qur-aan na Sunnah. Lakini wanazuoni wamekubaliana wote katika kuwasimanga na kuwatia upotofuni, japokuwa wametofautiana katika kuwakufurisha au kutowakufurisha.
Ikiwa mwenye kutaka haki atajua kwamba hizi tafsiri mbovu walizonazo ni za al-Mariysiyyah zilizotokana na kutafsiriwa kwa vitabu vya warumi katika zama za al-Ma’muun, basi haki itambainikia – ikiwa kweli anaitaka haki. Ama yule asiyeitaka haki, basi hoja imeshasimama juu yake. Katika zama zetu wamepatikana watu wanaowatukuza hawa wapotofu na makafiri na wanamdharau yule anayewaraddi na kubainisha batili yao. Kila watu wana mrithi na watu wana njia mbalimbali katika vile wanavyovipenda.
Fatwa hii ambayo Shaykh ameandika ikiwa ni jawabu kwa aliyemuuliza kuhusu ´Aqiydah ya wanazuoni katika majina na sifa, si mahali pa kurefusha na kufafanua kwa kirefu. Huu ni udhuru kutoka kwake (Rahimahu Allaah) kuhusu kutopanua maelezo, kwa sababu fatwa inatakiwa iwe kwa kifupi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 194-195
- Imechapishwa: 07/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Aidha wanapoona namna ambavyo maimamu waliafikiana katika kumsema vibaya Mariysiyyah, wengi wao walimkufurisha au wakampita upotofuni na kwamba yale yanayosemwa na hawa waliokuja nyuma ndio yaleyale yaliyosemwa na Mariysiyyah, basi utabainika uongofu kwa yule ambaye Allaah anataka kumwongoza. Hata hivyo makusudio ya fatwa hii sio kuingia kina ndani mada hii, nitaashiria kanuni za mambo peke yake. Mwenye busara ataangalia na kutafiti mwenyewe.
MAELEZO
Baadhi ya wanazuoni waliwakufurisha Jahmiyyah kwa sababu ya imani yao ya ukafiri na upotofu. Baadhi yao hawakuwakufurisha wale wanaowafuata kichwa mchunga, lakini waliwahukumu kuwa wamepotea. Ama yule anayekuwa mwanachuoni miongoni mwao na anakusudia kuwapotosha watu, basi huyo ni kafiri bila shaka. Kwa sababu ni mwenye kufanyia inadi Qur-aan na Sunnah. Lakini wanazuoni wamekubaliana wote katika kuwasimanga na kuwatia upotofuni, japokuwa wametofautiana katika kuwakufurisha au kutowakufurisha.
Ikiwa mwenye kutaka haki atajua kwamba hizi tafsiri mbovu walizonazo ni za al-Mariysiyyah zilizotokana na kutafsiriwa kwa vitabu vya warumi katika zama za al-Ma’muun, basi haki itambainikia – ikiwa kweli anaitaka haki. Ama yule asiyeitaka haki, basi hoja imeshasimama juu yake. Katika zama zetu wamepatikana watu wanaowatukuza hawa wapotofu na makafiri na wanamdharau yule anayewaraddi na kubainisha batili yao. Kila watu wana mrithi na watu wana njia mbalimbali katika vile wanavyovipenda.
Fatwa hii ambayo Shaykh ameandika ikiwa ni jawabu kwa aliyemuuliza kuhusu ´Aqiydah ya wanazuoni katika majina na sifa, si mahali pa kurefusha na kufafanua kwa kirefu. Huu ni udhuru kutoka kwake (Rahimahu Allaah) kuhusu kutopanua maelezo, kwa sababu fatwa inatakiwa iwe kwa kifupi.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 194-195
Imechapishwa: 07/07/2026
https://firqatunnajia.com/121-aqiydah-ileile-kama-ya-al-mariysiy/