Mali ya mke anayomuazima mume wake

Swali: Nilimnunulia mke wangu dhahabu. Wakati nilipohitajia kiwango cha pesa akaniuzia kwa ridhaa yake na nikatumia mali hiyo. Je, ni lazima kwangu kumrudishia wakati atakaponiomba hilo?

Jibu: Ikiwa ameikupa na akakuruhusu [kuitumia], sio wajibu kumrudishia. Ama ikiwa ameikupa kwa sharti umrudishie nayo [baadaye] au umrudishie kiwango badala yake, ni wajibu kumrudishie. Isipokuwa tu ikiwa kama atakusamehe.

Check Also

Peleka mahakamani

Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, …