Makusudio ya kukaribiana kwa zama

Swali: Kukaribiana masoko ni katika alama za Qiyaamah?

Jibu: Imekuja katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba zama zitakaribiana. Kuhusu masoko ni maneno tu ya watu. Alama za Qiyaamah ni kukaribiana kwa zama, mauaji yatakuwa mengi na pombe zitanywiwa kwa wingi. Yote haya yatakuwa katika zama za mwisho. Ameyaeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyokuja katika al-Bukhaariy na kwenginepo.

Swali: Ni nini makusudio ya zama kukaribiana?

Jibu: Bi maana mwaka utakuwa kama mwezi, mwezi utakuwa kama wiki na wiki itakuwa kama siku moja. Kwa  maana nyingine wakati utaenda haraka sana na baraka itakuwa chache.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22666/هل-تقارب-الاسواق-من-علامات-الساعة
  • Imechapishwa: 13/07/2023