94 – Ibn Mishar ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ibraahiym bin al-Muhaajir, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, aliyesema kuwaambia watumwa wake:

”Yeyote katika nyinyi anayetaka kuoa basi tutamuozesha. Hakuna yeyote miongoni mwenu atakayezini isipokuwa Allaah humwondoshea nuru ya imani. Akitaka anairudisha, na Akitaka kumnyima nayo basi anamnyima nayo.”[1]

95 – Qabiysah ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Ibn Twaawuus, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Ajabu iliyoje kwa ndugu zetu wa ´Iraaq ambao wanamwita al-Hajjaaj kuwa ni muumini.”[2]

96 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur, ambaye ameeleza:

”Wakati alipokuwa akitajwa al-Hajjaaj, basi alikuwa akisema:

أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ

”Zindukeni! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu.”[3][4]

97 – Abu Bakr bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa al-Ajlah, kutoka kwa ash-Sha´biy, ambaye amesema:

”Nashuhudia ya kwamba ni mwenye kuchupa  mipaka[5] na mwenye kumkufuru Allaah.”[6]

Bi maana al-Hajjaaj.

98 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, ambaye amesema:

”Inatosha kwa ambaye anatilia shaka jambo la al-Hajjaaj – Allaah amlaani!”[7]

99 – Yahyaa bin Aadam ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Aaswim, ambaye amesema:

”Tulimwambia Twalq bin Habiyb: ”Tueleze kuhusu kumcha Allaah.” Akasema: ”Kumcha Allaah ni kutendea kazi kumtii Allaah hali ya kutaraji rehema za Allaah, kutokana na nuru kutoka kwa Allaah. Kumcha Allaah pia ni kuacha kumuasi Allaah kwa ajili ya kumuogopa Allaah, kutokana na nuru kutoka kwa Allaah.”[8]

100 – Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin Abiy Bashiyr, kutoka kwa ´Abdullaah bin Musaawir, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Si muumini yule mwenye kulala hali ya kuwa ameshiba na jirani karibu yake yuko na njaa.”[9]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Wapokezi wake ni waaminifu na ni wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim – wote isipokuwa Ibraahiym bin al-Muhaajir al-Bajaliy al-Kuufiy, ni katika wanamme wa Muslim peke yake. Alikuwa mkweli na msimuliaji laini, kama ilivyo kaitka “at-Taqriyb”. Imekwishatangulia (71) kwa cheni ya wapokezi nyingine.  

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[3] 11:18

[4] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[5] Bi maana shaytwaan.

[6] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[7] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[8] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwenda mpaka kwa Twalq bin Habiyb, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Maswahabah mfanya ´ibaadah.

[9] Swahiyh kupitia Hadiyth zingine zinazoitia nguvu. Nimeitaja katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (148).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 13/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy