Makatazo ya kuswali kwenye misikiti ilio na makaburi

Swali: Baadhi ya wale wanaojidai kuwa na elimu wanasema ya kwamba inajuzu kuswali kwenye misikiti ilio na makaburi na makuba. Vipi mtu atajibia hili?

Jibu: Aliyesema hivi ima hajui makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kuswali kwenye makaburi na kuyafanya kuwa ni mahala pa kuswalia au anajua hili na ni mkoseaji. Hakuna hoja kwake. Sisi tunafuata maneno na makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kuswali kwenye makaburi na kuyafanya kuwa ni mahali pa kuswalia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020