Ukimaliza kusoma rudi katika mji wako ukalinganie watu Tawhiyd

Swali: Je, ni wajibu kwa wanafunzi kurudi katika miji yao walipotoka ili wawalinganie watu katika dini ya Allaah (Ta´ala) na katika Tawhiyd yake?

Jibu: Hili halina shaka. Hili ni wajibu kwao. Ikiwa wanaweza ni wajibu kwao kufanya hivi.

وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“… na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

Ikiwa wanaweza kufanya hivi, hili ndio la wajibu kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020