Swali: Kuna mtu anaridhia shirki kubwa ya kuyaomba makaburi na kuyawekea nadhiri. Anatetea hili kutokana na nguvu zake na anamtia jela yule anayewakataza washirikina hawa. Sambamba na hilo anawabania wale wanaolingania katika Tawhiyd katika mji wake ambapo anaishi. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Ni juu yenu kuwa na subira na kusimama kwa kulingania kwa kiasi na vile mnavyoweza na lile mnaloliweza mpaka pale ambapo Allaah Ataleta faraja.

Mimi naonelea lau walinganizi wangeliwaendea watawala na kuwalingania na wakawa na ukaribu nao, huenda Allaah Angeliwafanya wakaitikia au angalau kwa uchache wakasitisha shari zao [za waabudu makaburi]. Lakini ikiwa walinganizi watakuwa upande huu na watawala upande mwingine, ndio hutokea shari kati ya watawala na walinganizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020